Hostel

MRADI WA Hostel

Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na vitega uchumi vingine kuweza kusaidia matoleo ya kanisa, wakristo wa usharika huu walifikia maamuzi ya kuanzisha mradi wa hostel ambao unapatikana karibu na eneo la kanisa. Mradi huu ulianza kufanya kazi mnamo November 2020 na ni mradi wenye jumla ya vyumba 9 self-contained Na Vilivyo katika hali nzuri na safi. Huduma hii ya malazi hupatikana kwa siku zote yaani kuanzia jumatatu hadi jumapili kwa kukaribisha wageni mbalimbali kutoka maeneo tofauti hapa nchini na nje ya nchi. Ujenzi wa Jengo la Hosteli ambalo lilianza Mwaka 2009 chini ya Mchungaji George Pindua na Kuendelezwa na Mchungaji Frank Bogasi hadi mwaka 2019. Jengo hili lilikamiliaka chini ya mchungaji Joyce Msuya mwaka 2020 na kufunguliwa Askofu wa Dayosisi ya Morogoro Jacob Mameo Ole Paul.

PICHA ZAIDI